Dude apata ajali, akimbizwa Hospitalini

 


Msanii wa filamu Bongo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amekimbizwa Hospitali ya Magomeni Jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya bodaboda kwa kugongwa na gari la kubebea wagonjwa Ambulance.

  • TAZAMA VIDEO HIII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WADAU SAPORT YENU  MUHIMU SANA NAWATEGEMEA WADAU WANGU WA NGUVU

Katibu wa wasanii wa filamu Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha kichwani.


"Kwa sasa tupo Hospitali Magomeni, alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na Ambulance yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali, mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo" ameeleza Katibu wa wasanii Jafari Makatu 

Comments