Ushuhuda wa Wanawake Waliotekwa, Kubakwa na Kugombolewa DRC


Wanawake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameliambia shirika la waangalizi wa haki za binaadamu madhila waliyoyapitia ya kutekwa nyara kwa ajili ya kupata fedha. vitendo vilivyotekelezwa na magenge ya wahalifu

Wengi wa walioshikiliwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita walitekwa wakiwa mashambani walikokuwa wakifanya kazi zao, kisha wakashurutishwa kutembea saa kadhaa kuelekea hifadhi ya taifa ya Virunga, eneo la urithi la shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi na utamaduni UNESCO, ambako walikuwa wakishikiliwa na kupigwa.

Kisha waliwasiliana na familia za wanaowashikilia na kuwataka kutoa fedha ili wawaachilie.

''Walituonesha mifupa ya binadamu na kusema kuwa ni watu waliowaua baada ya kukiuka amri zao,'' alisema manusura Yolande.

''Kuna nyakati walizima simu zao ili kuongeza shinikizo kwa familia hizo kwa kuwa hawakufurahia ofa zilizokuwa zikitolewa. Mateka wa kiume walipigwa vibaya zaidi.''

Wanawake na wasichana walikuwa wakibakwa kila siku mara nyingi kando na wanaume, ambao hukaa wakiwa wamefungwa na kamba kwenye mikono na miguu.

''Watu walioniteka walikuwa wanaipigia simu familia yangu huku wakinibaka ili wazazi wangu wasikie nikipiga kelele; walitaka wajue ni kiasi gani tulikuwa tukipata taabu na kuhakikisha kuwa wanatoa kikombozi,'' alisema Sarah ambaye alikuwa na miaka 18 na mwenye uja uzito wa miezi mitatu alipotekwa nyara.

Watu walikuwa wakishikiliwa kwa wiki moja mpaka siku 10 bila kupata chochote.

Walionusurika na vitendo vya udhalilishaji wa kingono wameathirika kiakili na kujeruhiwa, wakipata msaada mdogo baada ya kuachiwa.

Mara nyingi wenza wao wamekuwa wakiwatelekeza au kusema kuwa wamekuwa wakidharauliwa.

Monique amesema kuwa mume wake bado anamlaumu kwa changamoto ya fedha na kukataa kumpa pesa kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na kulipa gharama za matibabu yake: ''Hujibu pesa yetu yote tumelipa kikombozi.''

TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WADAU SAPORT YENU MUHIMU



Katika matukio takribani 170 yaliyoripotiwa kwa shirika la waangalizi wa haki za binadamu , pesa iliyolipwa kati ya dola za Marekani 200 mpaka 600 kwa kila mateka.

''Wazazi wangu waliuza shamba na mbuzi wetu pekee wa mwisho. Waliuza gunia la maharage tulilokuwa nalo nyumbani. Walichukua mikopo kutoka dukani na kanisani....tunateseka sana,'' Elizabeth alisema.

Wengi walionusurika wamesema polisi hawakuwahoji walipoachiwa huru- hivyo wanahisi hakuna matumaini ya kupatikana kwa haki.

Comments