Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.
Kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.
- TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU
Kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.
Imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k
Wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.
Comments
Post a Comment