Usitafsiri Vibaya HURUMA ya Mwanamke Kama ni Udhaifu Wake

Hii ni kwa ajili ya wanaume wote ambao wamekuwa na tabia ya kudharau pale mwanamke anapumuonesha huruma na upole.

Mwanamke akipenda kweli yu-radhi kukufanyia lolote lile! Atakuvumilia kwa kila hali, inabidi kutambua huruma na upendo wake ili kumtia nguvu.

  • TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU


Atapokupa dhati ya upole na huruma yake kisha wewe ukamlipa dharau na kuona umemuweka kiganjani,basi huruma hiyo hufika ukomo.

Moyo wa mwanamke ukiamua kukatia tamaa basi tambua hakuna kitu waweza fanya ukamrejesha katika hali yake ya awali.

Thamini jitihada za mwenzi wako anazokuonesha, zichukulie kwa uzito usije ukawa wewe ndiye sababu ya kuona kuwa hafai na hajitoshelezi!

Comments