Z Anto Aendelea Kumlilia Binti Kiziwi.."Tulioana Alafu Nikampa TALAKA Tatu Kwa Hasira Kimakosa"

“Mimi na Sandra Khan (Binti kiziwi) tulifunga ndoa ila nilimpa talaka kabla hata hajafungwa China, tena nilizitoa kimakosa na kwa hasira nikatoa tatu kwa pamoja, hatukuwahi kuwa na Mtoto, naamini tuliachana sababu ya utoto, nilimuoa akiwa mdogo na mie sikuwa nimepevuka”- Z Anto

  • TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE

“Nimeamua kumuweka tena Binti Kiziwi kwenye video ya wimbo wangu mpya wa ‘Nichape’ kwasababu muda alioupoteza akiwa jela China ni mwingi, alifahamika kupitia Muziki nikaona nimrudishie hadhi yake na jina lake, itamsaidia kufanya biashara zake nyingine kama saloon nk”- Z Anto

Comments