Zijue Sifa za Watu Wenye Mafanikio


Je unataka kuwa mtu wa mafaniko? Je unazo sifa muhimu kukusaidia kufanikiwa? Unataka kufanikiwa? Ikiwa unafikiri kama watu wengi waliofanikiwa basi zipo sifa 6 za mafanikio walizonazo watu wenye mafanikio:

Wanayo matamanio pamoja na nia pia.
Wanajiona wenyewe na kujiamini kuwa na uwezo wa kufanya vizuri na kuwa wako vizuri katika eneo lao. Ni rahisi sana kumwona mtu ambaye anafanya vizuri zaidi yako na kufikiri kuwa huwezi kufika mahali ukafanya vizuri kama yeye huo ni uongo mtupu.

Jambo la msingi kukumbuka ni kwamba waliofanikiwa wanakujua kushindwa kwa sababu wao waliwahi kuwa waathirika wa kushindwa. Iwe kushindwa maisha,masomo au biashara wameishi kushindwa.

Ni jasiri.
Maadui wawili wakubwa wanaoshikilia watu wengi washindwe kufikia mafanikio ni hofu na uoga. Watu wanofanikiwa wana ujasiri mkubwa wa kukabili aina yoyote ya uoga katika shughuli na maisha yao ya kila siku.

Unaporudia kufanya kitu kwa muda mrefu unajenga tabia hivyo kwa kuongozwa na hofu na uoga unajenga tabia ya uoga na mashaka. Kama utaamua kufanya yale unayoogopa ni dhahiri utakuwa umeua mashaka na uoga.

Huwa wanajitoa kwa moyo wote.
Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali wanajitoa kikamilifu kutimiza kile wanachotaka kutimiza. Wanaamini kazi na kampuni zao, wanajiamini, wanaamini katika bidhaa na huduma zao, wanaamini wateja wao.

Bila shaka tunajua kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya unavyoamini na uhalisia. Kwa hiyo kama unaamini katika usahihi na uzuri wa kile unachofanya unajenga kile kinachoitwa uhamisho.Unahamisha imani kwenye vitu vinavyoonekana kwa njia ya marudio.Watu wasiotaka kujitoa hujikuta wanaishi maisha matupu.

Hujiandaa.
Watu waliofanikiwa hupitia kila kitu mapema kama hatua ya kujiridhisha. Wanafanya mambo ambayo mtu wa kawaida hayuko tayari kufanya.

Kabla hujaenda kwenye kikao kwa mfano fanya kazi yako ya nyumbani. Kabla hujatoa hotuba hakikisha tafiti taarifa na kufanya mazoezi ya kuongea kabla ya kwenda kuanza.

Ni wanafunzi endelevu.
Watu wanaofanikiwa sana wana tabia ya kuwa wanafunzi wasiokoma. Siku zote wanahangaika kutafuta marifa zaidi kwa hiyo hawezi kutulia maana wanajua kama wakisimama kuwa wazuri kwenye eneo wanalofanya basi.

Kwa hiyo wanasoma vitabu, wanasikiliza CD, na wanahudhuria mafunzo. Wataalam hata siku moja hawakomi kuendela kujifunza. Kama unataka kufanikiwa usiache kuwa mwanafunzi kula siku.

Wanawajibika.
Watu wengi walio juu wana tabia ya kujiajiri wenyewe. Hii ni muhimu sana kwa sababu 100% ya watu waliofanikiwa wako katika sekta binafsi. Tunafanya kazi kwa ajili yetu lakini tatizo kubwa ni pale unapofikiri kuwa unafanya kazi kwa ajili ya watu wengine. Watu waliofanikiwa wana sifa ya kuwajibika wenyewe kwa mema na mabaya bila kusukumia watu wengine.

Comments