Jambo usilolijua kutoka kwa Madee na Rayvanny


Msanii wa Muziki, Madee amefunguka kama kuna mawasiliano kati yake na RayVanny baada ya kuwahi kufanya nae kazi Tip Top Connection alipoanzia.

"Mahusiano ya way back na sasa hivi hayawezi kuwa sawa, mimi plan zangu nikuona mtu anaendelea kwenye maisha yake yaani anatimiza kile anachokiota, Mwanzo lazima mahusiano yawe karibu sana kwasababu tunalala wote tunaamka wote tunawasiliana muda wowote," alisema Madee.

"Kwasasa hivi lazima kuwe kuna vitu vinapungua,kwasababu sasa hivi hawezi kunipigia simu kuniomba 2000, 3000 kwasababu anayo, sasa hivi hawezi kunipigia simu kuniomba gari kusema aende sehemu fulani kwasababu analo lakini heshima bado iko pale pale ananiheshimu na anaheshimu kila kitu kilichotoka kwangu hakuna kitu chochote kilichobadilika."

Kwasasa Rayvanny ni msanii aliyesainiwa kwenye lebo ya WCB Wasafi iliyo chini ya msanii Diamond Platnumz.

Comments